Monday, December 14, 2015

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ENG. RAMO MATALA MAKANI AANZA KAZI RASMI LEO KATIKA OFISI YAKE MPYA MPINGO HOUSE

Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Matala Makani 
(kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (katikati) ofisini kwake leo tarehe 14 Desemba 2015 baada ya kufika kwa mara ya kwanza toka kuteuliwa kwake na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo. Katika salam zake kwa uongozi na watumishi wa Wizara hiyo amewaomba ushirikiano wa dhati kwa kila mmoja kutekeleza majukumu yake kwa wakati ili kuleta maendeleo katika sekta ya Maliasili na Utalii nchini. Ameongeza kuwa yeye binafsi hawezi kuleta maajabu Wizarani hapo bila kupewa ushirikiano katika kazi. Pichani kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Ndugu Selestine Gesimba.   
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akitoa taarifa fupi ya muundo pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mhe. Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Ramo Matala Makani muda mfupi baada ya kuwasili katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Matala Makani 
(kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru wakati akimpa taarifa fupi ya muundo wa Wizara hiyo leo tarehe 14 Desemba 2015 . 
(Picha na Hamza Temba wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...