Wednesday, December 16, 2015

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKAGUA HUDUMA ZA AFYA MUHIMBILI

um1
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Ally Mwalimu akiingia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo asubuhi kwa ajili ya kukagua utengenezaji wa mashine ya MRI na CT- Scan.
um2
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru leo asubuhi katika hospitali hiyo.
um3
Mtaalamu wa Mionzi kwenye chumba cha mashine ya MRI,  Job Joshua (kushoto) na Profesa Mseru (wa pili kulia) wakimpatia maelezo Waziri Ummy Mwalimu (katikati) wakati alipotembelea leo hospitali hiyo kukagua utengenezaji wa mashine hiyo. 
UM4
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kwa Mheshimiwa Waziri kuhusu maendeleo ya utengenezaji wa mashine ya MRI leo asubuhi.
UM5
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu (katikati) akiwa na Profesa Mseru kuelekea kwenye chumba cha X-ray cha digitali.
UM6
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare (wa kwanza kulia) akimpatia maelezo mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (katikati) kuhusu utengenezaji wa mashine hiyo leo asubuhi.
UM7
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akizungumza leo asubuhi na wagonjwa wanaosubiri vipimo katika hospitali hiyo.
UM8
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika chumba cha CT-SCAN, huku Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akimpatia maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi wakati ikiwa nzima.
UM9
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akifafanua jambo baada ya kupewa maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
UM10
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Lawrence Mseru (kulia), Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (katikati) wakimsikiliza mgonjwa aliyefika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu leo asubuhi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...