Monday, December 14, 2015

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AWAAGIZA WAKUU WA IDARA KUANDAA TAARIFA ZA IDARA ZAO.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akizungumza na wakuu Idara katika wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi alipokutana nao leo alipokaribishwa kwa mara ya kwanza katika wizara  hiyo, tangu achaguliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa wizara, na kuwaagiza wakuu wa idara katika wizara hiyo kutoa taaarifa za idara zao ifikapo jumatatu ya wiki ijayo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akipokea ripoti ya wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Katibu mkuu wa wizara yaWizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Kidata. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula. 
Naibu Waziri wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akipokea ripoti ya wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo makazi leo walipokutana na wakuu wa idara mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi.
Naibu Waziri wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akizungumza na wakuu wa Idara wa wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam, akizungumzia kuhusiana na wawekezaji ambao watakua hawajaendeleza ardhi ambayo walichukua kwa aajili ya uwekezaji na ardhi hiyo kurudishwa kwa wananchi. Kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi Nymba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Midata, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi  na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi, Nymba na Maendeleo ya Makazi, Selassie Mayunga.
Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wakuu wa Idara za wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...