Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II ikiwa nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar kabla ya kufunga gati Bandarini hapo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizaza ya Miundombinu waliofika Bandari Kuu ya Zanzibar kushuhudia kuwasili kwa Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II ikitokea Korea kusini.
Sehemu ya ndani ya Meli ya MV. MAPINDUZI II itakayotumika kwa ajili ya mapumziko kwa abiria watakao safari.
Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari juu ya matumizi ya gharama zilizotumika mara baada ya kuwasili kwa Meli ya MV. MAPINDUZI II Mjini Zanzibar.
Meli ya MV MAPINDUZI II yatia nanga Bandari kuu ya Zanzibar ikitokea Korea Kusini. Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………..
Na Maryam Kidiko Maelezo Zanzibar
Meli mpya ya Mv.Mapinduzi ( ii) imewasili bandarini Zanzibar kwa ajili ya kuanza safari zake baada ya kukamilika ujenzi wake huko Korea ya kusini.
Hafla ya kuwasili kwa meli hiyo imeongozwa na waziri wa fedha Omar Yussuf Mzee ambapo amesema ujenzi wa meli hiyo ni agizo la raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Amesema meli hiyo bado iko katika mikono ya wajenzi hadi sasa na inatarajiwa kuzinduliwa rasmin wiki ijayo na rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein ambaye ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Waziri mzee amesema meli hiyo inavifaa vya kutosha kama vile life jacket, pamoja na boti ndogo ili kuweka usalama kwa abiria wataosafiri katika meli hiyo.
Hata hivyo amesema meli hiyo itasafiri Pemba pamoja na Dar es-salaam hivyo amewataka wananchi kuitunza meli hiyo kwani ni matunda yao.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Miundo mbinu na mawasiliano zanizar Dk. Juma Malik amesema lengo kulifanya shirika la meli lifanye kazi kibiashara ili kuongeza pato la taifa.
Amewaomba wananchi kuitunza na kuitumia vizuri meli hiyo kwani wamefanya kazi kubwa na kutumia gharama hadi kufikia kukamilika kwa meli hiyo.
Sambamba na hayo amesema meli hiyo ina uwezo wa kupakia abiria wasiopunguwa 1,200 pamoja na tani za mizigo 200.
Meli hiyo mpya ya Mv.Mapinduzi ( ii) imetengenezwa Korea kusini na kugharimu jumla ya dola Mil.30.4 za Marekani ambapo ujenzi wake hadi kukamilika umechukua jumla ya miezi 18.
Meli hiyo mpya ya Mv.Mapinduzi ( ii) imetengenezwa Korea kusini na kugharimu jumla ya dola Mil.30.4 za Marekani ambapo ujenzi wake hadi kukamilika umechukua jumla ya miezi 18.
No comments:
Post a Comment