Tuesday, September 01, 2015

DK.SLAA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA SIASA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukaa kimya kingi sana tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo  chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia chama hicho. Leo ameibuka na kusema  ya moyoni kuwa amejivua uanachama  rasmi wa chama cha Chadema pamoja na Ukatibu Mkuuu wa Chama cha hicho na kuaachana  kabisa na siasa  kutokana na mambo yaliyokuwayakifanyika ndani ya chama chake hayakumlidhisha na hakukubaliana nayo.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa pia amesema kuwa mambo yaliyotokea katika chama chake ndio maana ameamua kuachana na siasa  rasmi hii leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.





Baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk.  Wilbroard Slaa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...