Daktari Bingwa wa magonwa ya moyo, Dk Tulizo Shemu (kulia) wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari katika taasisi hiyo kuhusu siku ya afya ya moyo duniani ambayo inafanyika Septemba 29, kila mwaka.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo nchini, Dk Tatizo Wane (kulia) wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari katika taasisi hiyo kuhusu siku ya afya ya moyo duniani ambayo inafanyika Septemba 29, kila mwaka. Kesho watu watapimwa bure shinikizo la damu na watakaopatikana na tatizo hilo watapewa ushauri wa bure. Pia siku ya kesho (Septemba 29, 2015) Taasisi hiyo itagawa vepeperushi, majarida na CD zinazozungumzia magonjwa ya moyo.
Baadhi ya waandishi wa habari.
SIKU YA MOYO, WANANCHI KUPIMWA SHINIKIZO LA DAMU BURE.
KATIKA kuazimisha siku ya afya ya Moyo Duniani Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- leo itatoa huduma ya upimaji wa shinikizo la damu bure pamoja na kuwashauri wale watakaopatikana na tatizo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya afya ya moyo Duniani ambayo huazimishwa Septemba 29 kila mwaka , Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo Tulizo Shemu kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kitwete amesema magonjwa ya moyo yanachangia asilimia 31 ya vifo vyote vinavyosababisha takribani watu MIlioni 17. 3 kufa kila mwaka .
Inasadikika itakapofika mwaka 2030 zaidi ya watu Milioni 25 watakuwa wanapoteza maisha kutokana na maradhi hayo hasa katika nchi zilizo na uchumi wa chini na kati.
Siku ya afya ya moyo Duniani hutoa fursa kwa watu wote Duniani kuazimisha kwa vitendo katika kujilinda na janga la magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ambayo yanachangia vifo vingi .
Dokta Shem ametaja baadhi ya visababishi vinavyochangia magonjwa ya moyo kuwa ni matumizi ya tumbaku, chumvi , pombe, vyakula vyenye mafuta, kutofanya mazoezi , unene uliokithiri , kutotibu ugonjwa wa kisukari na kuwa na mafuta mengi kwenye damu.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni kuweka mazingira mazuri ya afya bora ya moyo katika sehemu zetu tunazofanyia kazi kwa kuhakikisha kila mtu anatoa mchango katika kujenga afya bora ya moyo ili kupunguza visababishi vinavyochochea magonjwa hayo.
No comments:
Post a Comment