Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wahudhuriaji wa tamasha la ‘KiliFest’ wataweza kutumia Selcom Card kupata tiketi za tamasha hilo lililoandaliwa na kampuni ya Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambalo litafanyika siku ya Jumamosi September 26, 2015 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.
Kati ya mawakala wa Selcom zaidi ya 15,000 wanaopatikana nchi nzima ni mawakala 40 tu wameochaguliwa kuuza tiketi za KiliFest kwenye vituo vyao na wote hao wanapatikana Dar es salaam.
Baada ya kulipia Tsh 10,000/- tiketi itawekwa moja kwa moja kwenye Selcom Card kwa njia ya kielektroniki ambapo mteja atakuwa amepata Selcom Card bure na atatakiwa kufika na kadi hiyo Leaders Club siku ya tamasha na kugonga (tap) kwenye mashine za POS za Selcom zitakazokuwa zinapatikana kwenye milango ya kuingilia ya Leaders Club ili kuhakikisha manunuzi ya tiketi.
Selcom Card itamuwezesha mteja kupata tiketi za tamasha la KiliFest kwa sasa na kuitumia kadi hiyo hapo baadae kufanya malipo na manunuzi mbalimbali baada ya tamasha hilo.
Malipo na manunuzi yatakayoweza kufanyika kwa kutumia Selcom Card ni pamoja na malipo ya manunuzi ya bidhaa kwenye supermarkets, kulipia mafuta ya gari kwenye vituo vya mafuta, kulipia tiketi za matamsha yajayo, kulipia bili za chakula kwenye migahawa/bar, kupokea na kutuma pesa kwenda mitandao yote na kwenye akaunti za benki, kutoa pesa kwa wakala wa Selcom, kulipia tiketi za usafiri, bili za LUKU, DAWASCO, NHC, AzamTV, ZUKU, Startimes, DSTV, nk, kununua vifurushi vya internet pamoja na muda wa maongezi wa mitandao yote.
Hapo awali kumekuwa na changamoto kubwa wakati wa uuzaji wa tiketi za matamasha mbalimbali ambapo imekuwa ni vigumu kudhibiti wizi na tiketi feki, kwa kupitia mfumo huu mpya wa Selcom Card sasa waandaji wa matamasha wataweza kuzuia wizi wa tiketi na kuwa na uwezo wa kuuza tiketi mapema kabla ya tamasha na pia kuweza kujua nani ameingia kwenye tamasha hilo.
Lengo kuu la Selcom Card ni kuwarahisishia wananchi na kuwajengea utamaduni wa kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa kadi ambao ni wa haraka, salama na uhakika bila kubeba fedha mkononi kila wanapohitaji kufanya malipo au mununuzi. Watumiaji wataweza kuongeza fedha kwenye kadi zao za Selcom (Salio) kwa mawakala wote wa Selcom nchini au kwa njia ya simu banking.
Selcom ni kampuni inayoongoza katika utoaji wa huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya simu za mkononi na yenye uzoefu mkubwa kwenye nyanja ya Teknolojia nchini Tanzania na ndio msingi wa uendeshaji wa huduma ya kifedha kwa njia ya simu ikishirikiana na mitandao yote minne ya simu hapa nchini, benki zaidi ya 30 na vituo vya mauzo vya Selcom vinavyotumia mashine za POS vilivyopo zaidi ya 15,000 nchi nzima.
Pia Selcom ni wawezeshaji wa malipo na manunuzi ya huduma mbalimbali kwa washirika zaidi ya 50 kupitia simu za mkononi, simu banking na mawakala wake.
Selcom ni kampuni inayoongoza Tanzania kwa kuanzisha huduma za malipo ya kielektroniki katika miji mbalimbali ya Afrika Mashariki na ni kampuni ya kwanza kuzindua malipo na manunuzi kwa njia ya kadi nchini Tanzania.
Selcom, Tunakuwezesha Kwa Njia Ya Teknolojia
info@Selcom.net
SEHEMU ZINAPOPATIKANA TIKETI ZA KILIFEST
NO.
|
SHOP NAME
|
LOCATION
|
DECRIPTION
|
1
|
Village Super Market
|
Masaki
|
Sea Cliff House Branch
|
2
|
Village Super Market
|
Masaki
|
Chole Road Branch
|
3
|
Village Super Market
|
Mbezi Beach
|
Tank Bovu Branch
|
4
|
Shrijee Supermarket
|
Osterbay - Morogoro Store near Mohans
|
Osterbay Branch
|
5
|
Shrijee Supermarket
|
Masaki
|
Masaki Branch
|
6
|
Shrijee Supermarket
|
Kisutu - Mtendeni Street
|
Kisutu Branch
|
8
|
Shoppers Supermarket
|
Mikocheni - Shoppers Plaza
|
Mikocheni Branch
|
9
|
Shoppers Supermarket
|
Mbezi Beach - Kwa Street
|
Mbezi Beach Branch
|
10
|
A to Z Supermarket
|
Upanga - Ocean Road - Near Ocean Road Hospital
|
Ocean Road Branch
|
11
|
Imalaseko Supermarket
|
Posta - Pamba Street
|
Posta Branch
|
12
|
Koli Finance
|
Posta - J Mall/Habour View Tower/Samora Street
|
J Mall Branch
|
13
|
Puma Petrol Station
|
Kisutu - Jamuhuri Street
|
Kitumbini Branch
|
14
|
Bahamadi Shop
|
K/koo - Living stone/Agrey Street
|
Opposite Bakhressa Depot
|
15
|
Bahamadi Shop
|
K/koo - Mahiwa/Living Stone Street
|
Nearby Kariakoo Bazar Bulding
|
16
|
Habibu Shop
|
K/koo - Living stone/Pemba Street
|
Opposite Green Bureau Change
|
17
|
Crown and Beauty Shop
|
Mlimani City
|
In Mlimani City Mall
|
18
|
Big Bon
|
Sinza Mori
|
At the Big Bon Petrol Station
|
19
|
C - Park Cub
|
Kinindoni B
|
Kinondoni B nearby Bus Stop
|
20
|
Baby Face Internet Café
|
Mwananyamala (A)
|
Near bus stop of Mwannyamala A
|
21
|
Treenaz G.Supplies
|
Kawe - Mlalakuwa Street
|
Opposite EFM Radio
|
22
|
Jukas Shop
|
Africa Sana
|
Opposite Africana Shop near the Africana Market
|
23
|
Puma Petrol Station
|
Mbezi Bech Branch
|
Between Interchick and Tank Bovu Bus Stops
|
24
|
Petro Fuel Station
|
Tegeta Branch
|
Near Azania Bus Stop
|
25
|
Swai Shop
|
Ubungo Riverside
|
At kibangu Bus stop
|
28
|
Virus Internet Café
|
Magomeni - Magomeni Mapipa
|
Nearby Mapipa Bus Stop
|
29
|
Bakari Shop
|
Magomeni -Mwembe Chai
|
Neaby Bus Stop Opposite Mosque
|
30
|
Twaha Shop
|
Magomei – Kagera
|
Nearby Old Kagera Bus Stop
|
31
|
Eshanaa Classic Ware
|
Magomeni - Kagera
|
Opposite Oil Com Petrol Station
|
32
|
Elvis Digital & Network
|
Mbezi Louis
|
Dealer of DSTV opposite Old Bus Stop
|
33
|
Mohamed Shop
|
Mbagala Kongowe
|
Nearest to the Bus Stop of Tua Ngoma
|
34
|
Merseytel Shop
|
Mbagala Rangi Zakiem
|
Opposite Darlive Pub
|
35
|
Kipanga Stationery
|
Mtoni kwa Aziz Ally
|
Nearby Aljazira Supermarket
|
36
|
Khadija Shop
|
Mtoni kwa Aziz Ally
|
Nearest to the Mtoni kwa Aziz Ally Bus stop
|
37
|
No comments:
Post a Comment