Saturday, September 26, 2015

MWILI WA MAREHEMU CELINA O. KOMBANI WAWASILI DAR ES SALAAM MUDA HUU, WATUMISHI WA OFISI YAKE WAMLILIA


Pumzika kwa Amani mpendwa wetu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani (pichani enzi za uhai wake).
Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu na watumishi wote wa Ofisi ya Rais-Utumishi wataendelea kukukumbuka daima kwa busara zako na uongozi wako mzuri. Mola ailaze Roho yako 
pahala pema peponi - AMIN
-------------------------------------------------------------------

Wakati huo huo mwili wa Marehemu Celina O. Kombani umewasili muda huu katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Utaratibu wa msiba unasimamiwa na serikali na ofisi za Bunge. Tutaendelea kuwafahamisha ratiba kila tutapopata taarifa. 
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani umewasili muda huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
 Familia ya marehemu, viongozi mbalimbali na wananchi wakisubili mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ulipowasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Aliyeshikwa bega wa tatu kushoto ni Mume wa Marehemu Mzee Kombani.
 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukitelemshwa baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukipelekwa kwenye ambulance  baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukipakiwa  kwenye ambulance  baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge Mhe Anne Abdallah na viongozi wengine wakiwa Uwanja wa ndege kupokea mwili wa marehemu Kombani. 
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...