Tuesday, September 22, 2015

NYALANDU AZINDUA KAMPENI KATA YA MTINKO

 WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu,  akiingia kuzindua rasmi kampeni zake katika Uwanja wa Mtinko huku akisindikizwa na msafara mkubwa wa bodaboda.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu,  akisoma bango lenye ujumbe wa kumpongeza lililoandaliwa na wananchi wa Kata ya Mntiko, wakati wa uzinduzi wa kampeni zake za ubunge.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakicheza kwa furaha wakati wakiwasili kuzindua kampeni zake za ubunge katika Kata ya Mtinko.
  MKE wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Faraja, akicheza na wanachama na wapenzi wa CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni katika Jimbo la Singida Kaskazini, juzi.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, akihutubia umati wa wanachama na wakazi wa Kata ya Mtinko wakati uzinduzi wa kampeni zake, juzi.
 MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, mkewe Faraja na Mbunge mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, wakicheza muziki wa hamasa wa CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika Kata ya Mtinko, juzi
WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, akisalimia na mamia ya wanachama na wakazi wa Mtinko wakati alipozindua kampeni zake juzi, ambapo maelefu ya watu walijitokeza kumsikiliza

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...