Hizi ni nyumba za ghorofa za Mwongozo Beach Housing Estates ambao ni mradi wenye nyumba 216, zinavyoonekana kwa sasa.
Mwongozo Housing Estate imejengwa na kujitosheleza kwa huduma zake za
msingi kama zahanati, shule ya chekechea na maduka kwa ajili ya wakazi wake.
Mradi wa Mwongozo Housing Estate unatarajiwa kuchukua wakazi zaidi ya 1,000
kupitia nyumba 216 zinazouzwa.
Nyumba za Mwongozo Housing Estate zimetenganishwa sehemu mbili za
familia tofauti, moja ikiwa na vyumba viwili vya kulala na nyingine ikiwa na
vyumba vitatu vya kulala, jiko la kisasa, sebule kubwa na mahali pa kulia
chakula. Pia kila nyumba inayojitegemea na ina eneo kubwa la maegesho ya
magari. Nyumba zinajengwa kwa kuzingatia
vigezo vya kimataifa ili kumuwezesha mnunuzi kufurahia maisha ndani ya nyumba
ya kisasa.
No comments:
Post a Comment