Friday, September 25, 2015

GLOBAL EDUCATION LINK (GEL) YAZIDI KUPATA MAFANIKIO YA KUSAFIRISHA WANANFUNZI WAPATAO 70 NCHINI CHINA

IMG_2144
Mapema jana Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi waliweza kusafirisha wanafunzi wapatao 70 kwenda nchini China kwa ajili ya masoma. Akizungumza Mkurugeni wa GEL, Abdulmaliki Mollel alisema kuwa wanamshukru Mungu kwa kuendelea kuwafungulia milango ya kuendelea kupokea wanafunzi wanaopenda kusoma vyuo nje ya nchi.
Pichani: inawaonyesha  wakiwa tayari katika mstari wa kukaguliwa ili waweze kuanza safari yao ya kwenda nchini China kimasomo.
IMG_2138
Mzazi kumuaga mwanae kwa bashasha.
Mwandishi wa Mlimani Tv akifanya mahojiano na mmoja ya wanafunzi anyekwenda kusoma chuo kikuu nchini China.
Mkurugenzi Msaidizi wa GEL, Zakia kulia akimhoji mwanafunzi endapo anavielelezo vyote vya kusafilia ikiwemo Passport na nyaraka nyingine za shule.
Mmoja ya wazazi akikagua nyaraka za mwanae kabla hajasafiri.
Mfanyakazi wa GEL, JacquelineMbise akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari kuelezea maandalizi yote ya safari.
Wafanyakazi wa GEL, wakijadili jambo.
Wafanyakazi wa GEL, wakiendelea mahojiano na wazazi pamoja na wanafunzi.
Wazazi waliotoka jijini Arusha wakiwa katika sura ya furaha kwa ajili ya kumuaga Kijana wao ambaye alikuwa akisafiri kwenda nchini China kwa masomo.
Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vya nchini China wakiwa Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam kungojea kuondoka. Wanafunzi hao wanaondoka nchini chini ya usimamizi wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi.
Wazazi wakipiga ya kumbukumbu pamoja na mtoto wao.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kumaliza kazi yao.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...