JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA (TAWA)
Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuujulisha umma kuwa, Bodi mpya ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife Authority -TAWA), imeteuliwa rasmi kuanzia tarehe 09 mwezi Septemba, 2015.
Katika uteuzi huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Rajabu SEMFUKO kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ambao wameteuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii ni Dkt. Simon Mduma – Mkurugenzi Mkuu - TAWIRI, Dkt. Fred Manongi – Mhifadhi Mkuu - NCAA, Suzane Charles Ndomba – Mwanasheria – ATE, Bw. Gerald Bigurube – Meneja wa Program Frankfurt Zoological Society – SERENGETI, Dkt. David Manyanza (Mstaafu) Mtaalam wa Maswala ya Wanyamapori , Bw. Benson A. Shallanda – Kamishna wa Sera – HAZINA, Jenerali Samweli Ndomba – Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Winfrida Nshangeki – Mkurugenzi wa Uratibu wa Sera – TAMISEMI, Abdulrahman Kaniki – Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania , Allan J. Kijazi – Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mr. Herman W. Keraryo –Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori , Abdul Rajab Mhinte – Mkuu wa Idara ya Usalama na Atakayeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka.
Bodi hii, itaongoza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe ya uteuzi.
Imetolewa na
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali
Wizara ya Maliasili na Utalii
21/09/2015
No comments:
Post a Comment