Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (katikati), akiwakabidhi wawakilishi wa kikundi cha MIRANACO mjini Mbeya vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia katika biashara yao ya ufugaji wa nyuki. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa kwa kupatiwa mizinga ya nyuki, mashine za kukamulia asali, vifaa vya kinga ya nyuki na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki. Wakishuhudia kutoka kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha FURSA Irine Paul akifuatiwa na Meneja mauzo wa Airtel mkoani Mbeya Saidi Zani
Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (katikati), akiongea na wawakilishi wa kikundi cha MIRANACO katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia katika biashara yao ya ufugaji wa nyuki vikiwemo mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia asali 1, vifaa vya kinga ya nyuki 2, chupa za lita 1 400, chupa za asali za lita 5, 200 na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki mjini Mbeya . Wakishuhudia kutoka kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha FURSA Irine Paul akifuatiwa na Meneja mauzo wa Airtel mkoani Mbeya Saidi Zani.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@2
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imewawezesha vijana wajasiriamali wa kikundi cha MINARACO kutoka mkoani Mbeya wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki. Kikundi hicho kinaundwa na vijana 76 walioamua kuungana na kujihusisha katika ufugaji wa nyuki ili kujikwamua na changamoto za maisha. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa kwa kupatiwa mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia asali 1, vifaa vya kinga ya nyuki 2, chupa za lita 1, 400, chupa za asali za lita 5, 200 na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema, “vitendea kazi waliopatiwa ni vyakisasa zaidi na vitasaidia kuboresha ufugaji huo na kuwawezesha vijana hao kupata mavuno zaidi ya waliokuwa wakipata awali”.
Akiongezea amesema, “mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali vifaa ni sehemu ya mpango wa kampuni ya Airtel wa kuwawezesha vijana ili kuboresha maisha yao na ya watu wanaowazunguka”.
“Sisi kama Kampuni ya mawasiliano tumeona ni vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa mafunzo na vifaa” alisema meneja huyo”.
Wakipokea msaada huo wameishukuru, Airtel kwa kujitoa kwa kuwasaidia vijana katika kutatua changamoto zinazowakabili na kuahidi kutumia vifaa hivyo kwaajili ya kuongeza uzalishaji ili kufikia malengo waliojiwekea katika kikundi hicho.
“Hatukuamini kuwa Airtel itakuja kututembelea, kuangalia mahitaji yetu na hasa kwa kutupatia msaada wa vifaa vya kisasa walivyo tupatia leo, tunawashukuru sana na tunaahidi kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha tunakuza na kuendeleza ufugaji bora wa nyuki” alisema mwakilishi wa kikundi hicho John Maige.
Akiongezea Maige alisema, “Awali tulikuwa na changamoto ya uchache wa mizinga, vifungashio vya asali na soko la uhakika, lakini Airtel imetusaidia kwa kutupa mafunzo na vifaa vya kutosha vitakavyo tusaidia kupata Asali ya kutosha na yenye ubora mzuri “.
Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana.
No comments:
Post a Comment