Wednesday, September 30, 2015

MO KUANZISHA BENKI YA MIKOPO KWA WAFANYABISHARA WADOGO NCHINI

DSC_0316CEO wa Kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akiwa ofisini kwake.

………………………………………..
Na Modewjiblog team
Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji ambaye hivi karibuni amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015) amebainisha kuwa lengo kuu la kampuni anayoiongoza ya MeTL Group, hadi kufikia mwaka 2022, ni kufikia dola bilioni 5 huku akitarajia kuajiri wafanyakazi zaidi ya Laki moja.
Dewji maarufu kama MO amebainisha hayo wakati wa mahojiano maalum ya moja kwa moja yaliyorushwa hivi karibuni na kituo cha BBC kupitia kipindi cha BBC SWAHILI DIRA YA DUNIA ambapo alibainisha hayo.
Kupitia kipindi hicho cha BBC Swahili, MO aliweza kuelezea mafanikio aliyofikia ikiwemo siri ya kufanya kazi kwa bidii na kujituma.
Ambapo ameeleza kuwa, alianza biashara akiwa mdogo sana kwani wakati huo Baba yake alikuwa akimfundisha kazi na yeye kujituma zaidi bila kuchoka.
Aidha, MO amebainisha kuwa, yupo mbioni kuanzisha Benki ya kuweza kutoa mikopo midogo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kujiendeleza.
DSC_0310Salim Kikeke aliweza kumuuliza swali juu ya vijana wengi wanapenda kufanyabiashara lakini hawana mitaji ambapo MO alifunguka kuwa:
“Unajua na mimi mwenyewe nataka kuanzisha ‘Micro credit bank’, ya kuweza kutoa mikopo midogomidogo kwa wafanyabiashara wadogo. Kwa sasa hivi kuna benk nyingi sana zimezidi ukilinganisha mwaka 1998, nilipotoka Marekani, benki zilikuwa ndogo sana kwa hiyo nimeanza kutafuta pesa kutoka benki za Afrika Kusini” ameeleza MO na kuongeza kuwa mtu unapokuwa na wazo la kuanzisha biashara unaweza kushirikiana na mwenye pesa ama kukopa kwa mtu mwenye pesa. alifafanua MO .
Katika mahojiano hayo, MO alibainisha kuwa, mapato katika akaunti ya MeTL GROUP ina kiasi cha dola bilioni 1.3 huku akiwa ameajiri watu zaidi ya 24,000 huku lengo hadi kufikia mwaka 2022, kuwa na wafanyakazi zaidi ya Laki moja huku mapato kuwa zaidi ya dola bilioni 5.
Tuzo aliyopata MO alikabidhiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa na Helen Hai.
MO alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...