Sunday, September 27, 2015

MAGUFULI AWASHA MOTO SHINYANGA


 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Kambarage ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati umefika wa kujenga Tanzania mpya yenye viwanda vya kutosha kutoa ajira kwa vijana wengi.
Alisema pia kuwa Serikali yake itakuwa rafiki wa sekta binafsi na kuwajengea uwezo wafanya biashara ndogo ndogo ili waweze kujiendeleza.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Shinyanga kwenye mkutano wake wa Kampeni ambapo aliwaambai wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kufanya kazi zaidi kwa maendeleo ya nchi.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisiti za jambo wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Shinyanga mjini.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea
ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele kwenye mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Kambarage.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao Mgombea urais anazo changamoto za Shinyanga mjini na anaamini atazitatua hivyo amewataka watu wake kumpa kura nyingi za Dk. John Pombe Magufuli ifikapo tarehe 25 Octoba.
 Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini akihutubia wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Kambarage.
 Kikundi cha Ngoma za Asili kutoka Mwanza maarufu kwa jina la Mchele Mchele kikitumbuiza kwenye mkutano wa kumnadi mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdul Kiba akionyesha uwezo wake kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Shinyanga.
 Vijana kutoka Temeke jijini Dar es Salaam ,Chegge na Temba wakishambulia jukwaa pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele.
 Mwasiti akiimba wakati wa mkutano wa kampeni za CCM mkoani Shinyanga.
 Wasanii wakipiga push up jukwaani kabla ya mgombea wa urais kupitia CCM hajahutubia.
 Msanii wa muziki wa kufoka foka Mwana FA akishambulia jukwaa wakati wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Kambarage,Shinyanga mjini.
 Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaji Saad Kusilawe akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini na kuwaambia CCM ipo imara kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote hasa baada ya mizigo kuhama.
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM Mzee Samuel Sitta akihutubia wakazi wa mkoa wa Shinyanga kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah Bulembo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa mji wa Shinyanga mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Kambarage.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiteta jambo na mgombea ubunge wa jimbo la Solwa Ndugu Ahmed Ally Salum (kushoto)kabla ya kuwahutubia wakazi wa Solwa waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Solwa Joshoni.
 Wananchi wa Jimbo la Solwa wakimsikiliza Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitemkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM mgombea ubunge wa jimbo la Solwa Ndugu Ahmed Ally Salum (kushoto) kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Solwa Joshoni.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...