Thursday, April 16, 2015

ZITTO KABWE WA ACT AHUTUBIA SINGIDA

TOW7Zitto akiwahutubia wananchi Manyoni Mjini.
……………………………………………………………
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema kinaweza kuunganisha nguvu na yama vingine vya upinzani ili kukiondoa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao ambapo alisema shauku kubwa ya wananchi ni kutaka kujua msimamo wa ACT Wazalendo katika kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili kufanikisha malengo ya kuiondoa CCM katika madaraka.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Singida na Kiongozi wa ACT wazalendo Zitto Kabwe wakati akihutubia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi ukombozi.
“Tumedhamiria kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo  unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa”alisema na kuongeza
“ACT- Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu Alliance na msimamo wetu kuhusu mabadiliko ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.
Kiongozi huyo wa ACT alisema chama hicho hakina tatizo na kipo tayari kushirikiana na chama chochote kilichokuwa  tayari kushirikiana nao ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), 
Alisema umoja huo ni lazima uwe na malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.
Alikanusha chama hicho kutoa  kauli yeyote dhidi ya UKAWA kama inavyoaminishwa na baadhi ya watu, bali wameweka wazi kuwa lazima misingi ya kiitikadi na kifalsafa izingatiwe katika ushirikiano wowote
“Tupo tayari kwa umoja kwani ni moja ya misingi mikuu 10 ya chama chetu na umoja ni nguvu,” alisema Zitto.
Akizungumzia hali ya umaskini kwa mkoa wa Singida, Zitto alisema pamoja na hali ya umaskini Serikali ya CCM, imeshindwa kupunguza umasikini, nchini kwa kiasi kikubwa na kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Alisema ripoti ya maendeleo ya binadamu imeonyesha kuwa Tanzania imeshuka kufikia daraja la chini la nchi zenye kiwango kidogo zaidi cha maendeleo ya binadamu.
“Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya UNDP kuhusu Maendeleo ya Binadamu duniani ya mwaka 2014 ambayo imeiweka Tanzania katika kundi la nchi zenye maendeleo ya binadamu ya kiwango cha chini.  Lakini kinachoshitusha ni kushuka kwa nafasi saba zaidi katika Kipimo cha maendeleo ya binaadamu, (HDI), ukilinganisha na mwaka 2013.
“Ushahidi mzuri wa jambo hili ni ule unaotolewa na kipimo cha Maendeleo ya Binadamu (HDI), ambacho hupima maendeleo ya binadamu katika nchi kwa kuzingatia mkusanyiko wa vigezo vya umri wa kuishi, elimu na kipato,” alisema Zitto

No comments:

TANAPA YAMPONGEZA SIMBU; YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAE KUTANGAZA HIFADHI ZA TAIFA KUPITIA MCHEZO WA RIADHA

Na. Philipo Hassan, Arusha Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, CPA Musa Nassoro Kuji, amempongeza rasmi Sajini Taji Alphonce Simbu, bingwa wa D...