Kutoka kushoto ni Juma Herman(meneja wa Green Palm Hotel, Issaya Mwakilasa aka Wakuvwanga, Jhikolabwino Manyika, Kelvina John, Mwenyekiti Masoud Kipanya na Tonny Alphonce(Mtangazaji Metro fm 99.4
Siku ya Ijumaa ya tarehe 17/04/2015 ujumbe wa Imetosha Foundation ukiongozwa na Mwenyekiti Masoud Kipanya ulifanya mahojiano katika kituo cha redio cha Metro Fm 99.4 kwenye kipindi cha Pambazuko la Metro fm 99.4 ikiwa ni katika mfululizo wa kujitambulisha kanda ya ziwa kwa taasisi hiyo inayopinga mauaji kwa watu wenye ualbino kwa njia ya elimu.
Msanii wa vichekesho (comedian) Wakuvwanga ambaye ni mjumbe wa taasisi hiyo alitoa kali alipoulizwa angependekeza adhabu gani kwa watakaopatikana na hatia ya kuua watu wenye ualbino? akajibu "Kwa kuwa hawa si watu bali ni wanyama kutokana na vitendo vyao viovu basi napendekeza serikali iwapeleke Mikumi national park iwafungie ndani ya senyenge ili watalii wawe wanaenda kuwaona kama wanavyoenda kuwaona Simba na wanyama wengine! Kipindi hicho maridhawa kiliendeshwa na watangazaji Tonny Alphonce na Katumba Madua
|
Mtangazaji wa kipindi cha Pambazuko la Metro Fm, Tonny Alphonce akimuuliza swali Masoud Kipanya. |
|
Masoud Kipanya akijibu swali toka kwa mtangazaji wa Metro Fm 99.4zaji Tonny Alphonce. |
|
Tonny akimpiga swali Wakuvwanga, anayesikiliza kwa umakini wa hali ya juu, soma uone jibu lake! |
|
Kutoka kushoto ni Katumba Madua, Wakuvwanga na msanii wa muziki wa Reggae Jhikoman |
|
Moja ya studio za Metro Fm 99.4 ambazo wanazo tatu katika jengo hilo lililopo kati kati ya jiji la Mwanza |
|
Picha ya Pamoja ndani ya Metro fm 99.4 toka kushoto ni Juma Herman, Mkala Fundikira, Kelvina John, George Binagi, Tonny Alphonce, Rosier, Sophia George, Wakuvwanga Masoud na Katumba Madua. |
|
Jhikoman kushoto, Rosier(receiptionist) na Masoud. |
|
Masoud akibadilishana mawazo na Sphia George wa Metro fm 99.4 ya Mwanza wiki iliyopita ujumbe wa Imetosha Foundation ulipotembelea studio za kituo hicho cha redio. |
No comments:
Post a Comment