Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akianza mazoezi wakati akishiriki katika bonanza la Jogging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Jogging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gongo Gongo la Mboto kupitia Kipawa na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga ujumbe mkuu wa Bonanza hilo ulikuwa ni kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura kuliko kuwa mashabiki tu.
Bonanza hilo la mazoezi limeshirikisha vilabu mbalimbali vya Jogging kutoka mkoa wa Dar es salaam, Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (mwenye fulana ya rangi ya blu bahari) akikatiza mitaa ya Karakata wakati wa kushiriki jogging iliyoandaliwa na Kikundi cha Kaza Roho.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (mwenye fulana ya rangi ya blu bahari)akishiriki mazoezi ya jogging pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali yalioandaliwa na kikundi cha jogging cha KazaRoho kutoka Sitaki Shari.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (mwenye kofia nyeusi) akishiriki kikamilifu kukimbia mchaka mchaka na vijana zaidi ya 500 kutoka wilaya ya Ilala na Temeke.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea Ndugu Makongoro Mahanga wakati wa kupokea vikundi vya vijana kwenye viwanja vya Social ,Sitaki Shari .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea bendera ya Taifa kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha jogging Kaza Roho kama ishara ya kupokea vijana wa jogging kwenye viwanja vya Social Sitaki Shari jijini Dar Es salaam.
Vijana wakishiriki mazoezi ya Pamoja.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki pamoja na vijana kufanya mazoezi ya pamoja kwenye viwanja vya Social Sitaki Shari.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiruka kutoka jukwaani kuonyesha ukakamavu wakati wa mazoezi ya pamoja na vikundi zaidi ya 30 vya jogging kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari jijini Dar es Salaam.
Msaga Sumu akitumbuiza vijana wa mazoezi ya Jogging kwenye uwanja wa Social,Sitaki Shari.
Msanii wa siku nyingi ambaye alishawahi kuwa na kundi la Free Dogs Camp lililojuisha wasanii kama P wa Black, Nale Nale, OMG akitumbuiza kwenye bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kwenye viwanja vya Social ,Sitaki Shari.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wa jogging walishiriki bonanza maalum la kuhimiza wananchi wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kwenye viwanja vya Social,Sitaki Shari jijini Dar es salaam.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu vijana kwenye uwanja wa Social ambao walihudhuria bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura.
No comments:
Post a Comment