Thursday, April 30, 2015

TASWIRA ZA SUNDAY CELEBRATION SEASON 6 YA GWT

Waimbaji wa Glorious Worship Team (GWT) wakilishambulia jukwaa katika Sunday Celebration Season 6.
Kiongozi wa Bendi ya The Jordan, Daniel Mbepera, akiimba kwa hisia sambamba na bendi yake.
Wageni waliohudhuria wakisifu na kuabudu sambamba na GWT.
Mjasiriamali mahiri Afrika na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akitoa somo la ujasiriamali.
Wageni wakisikiliza somo la ujasiriamali kutoka kwa Shigongo.
Waimbaji wa GWT wakizidi kutoa burudani kwa washiriki wa Sunday Celebration Season 6.

KWA mara nyingine, kile Kikundi cha Kusifu na Kuabudu nchini cha Glorious Worship Team (GWT) Jumapili iliyopita kiliendelea na programu yake ijulikano kwa jina la 'Sunday Celebration' ambayo hufanyika kila Jumapili jioni.

Wiki iliyopita ilikuwa ni Sunday Celebration Season 6 ambapo burudani mbalimbali pamoja na elimu ya ujasiriamali vilitolewa kwa watu waliohudhuria katika Ukumbi uliopo Victoria Service Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Burudani ukumbini hapo ziliongozwa na Kundi la GWT likishirikiana na The Jordan Band huku elimu ya ujasiriamali ikitolewa na Mwalimu mahiri wa Ujasiriamali Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.
(PICHA ZOTE NA GWT)

1 comment:

Meizitang Botanical said...

thanks for sharing

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...