Tuesday, April 21, 2015

MADAKTARI BINGWA KUTOKA INDIA WATOA HUDUMA YA MATIBABU JIJINI ARUSHA

SAM_2087
Austin Makani  Mratibu wa Kambi ya matibabu Arusha katika kituo cha kutoa huduma kwa
wanawake (MMC)kilichopo mkabala na Hoteli ya Impala, akizungumza na waandishi wa habari  juu ya ujio wa madaktari bingwa kutoka India kwa ajili ya kuwaona wagonjwa wenye matatizo ya Moyo,Tumbo,Upasuaji wa saratani,Mishipa ya fahamu na uti wa mgongo,Shida za Figo,Mifupa,upasuaji wa jumla na upasuaji wa kupunguza uzito,zoezi hilo litafanyika kwanzia tarehe20-22 Aprili 2015(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_2071
Madaktari bingwa kutoka India
SAM_2085
Daktari bingwa kutoka India katika hospitali ya Apollo Abhijit Singh akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha katika kituo cha MMC Health
SAM_2088
Wagonjwa wakiwa wanapatiwa vipimo mbalimbali
SAM_2082
Atul Behll ambaye pia ni daktari bingwa kutoka India akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari
SAM_2097
Mgonjwa aliyekuja kupata huduma akiwa anasaidiwa na wahudumu wa kituo hicho
SAM_2084
Wagonjwa wakiwa wanasubiria kupata huduma
SAM_2091
Mmiliki wa mtandao wa http://jamiiblog.co.tz Pamela Mollel akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari bingwa kutoka India
SAM_2077
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kazini
SAM_2075
 
MADAKTARI bingwa kutoka hospitali ya  SPS Apollo iliyopo  Ludhiana
nchini India wamewasili nchini na kuanza kutoa huduma ya ushauri bure
kwa magonjwa makubwa ambayo yamekuwa yakiwasumbua watu wengi na
kuwalazimu  kwenda kutibiwa nchini India.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kutoa huduma kwa
wanawake (MMC) ambapo ushauri huo unatolewa, Mratibu wa Kambi hiyo ya
matibabu Arusha, Austin Makani alisema kuwa , madaktari bingwa hao
wanatoa ushauri kwa wagonjwa wenye matatizo ya Figo , Moyo, tumbo,
saratani, mishipa ya fahamu, uti wa mgongo, upasuaji wa kawaida na wa
kupunguza uzito.
Austin alisema kuwa,  ujio wa madaktari hao watano kutoka  nchini
India umeratibiwa na kituo  cha kutoa huduma kwa wanawake (MMC) kwa
kushirikiana na hospitali ya SPS Apollo iliyopo Ludhiana nchini India
na wamefikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa wagonjwa wengi
wanaoenda kutibiwa nchini India wanasumbuliwa na magonjwa hayo.
Alisema kuwa, uwepo wa madaktari hao bingwa kwa siku tatu utasaidia
sana wananchi wa jiji la Arusha kufika na kupewa ushauri bure juu ya
magonjwa yanayowasumbua na hivyo kuokoa gharama ya kusafiri hadi
nchini India kufuata huduma hizo.
‘hapa sisi wanachofanya madaktari hawa bingwa ni kusikiliza wagonjwa
na baada ya kupata maelezo wanapata ushauri bure wa kwenda kupima
kulingana na ugonjwa alionao na baada ya kurudisha majibu ndipo
tunamwandikia dawa ya kutumia na kama ugonjwa wake unahitaji kutibiwa
India tunampunguzia  gharama  kidogo ya kwenda kutibiwa India ‘alisema
Austin.
Alisema kuwa, uwepo wa kambi hiyo ya matibabu jijini Arusha unatoa
fursa pia kwa wagonjwa waliokuwa wakatibiwe nchini India kutokana na
magonjwa yanayowasumbua na kuweza kupata ushauri wa haraka na wakti
mwingine kuepuka gharama za kusafiri.
Wakizungumza  katika kituo hicho, Madaktari hao bingwa ,Abhijit Singh
na Atul Behll kutoka hospitali ya SPS Apollo India  walisema kuwa
,changamoto kubwa iliyopo katika nchi za kiafrika ni watu wengi
kutokuwa na utamaduni wa kwenda kupima afya zao ,hivyo aliwataka
wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kufika kwa wiki ili kupata
ushauri juu ya afya zao.
Walisema kuwa,nchini India  kuna watanzania wengi wanaopata matibabu
kutokana na magonjwa yaliyotajwa ,hivyo wakaona kuna umuhimu mkubwa
kwa wao kuwafikia na kuweza kutoa ushauri bure na hatimaye kupunguza
gharama za kwenda nchini India.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...