Thursday, April 23, 2015

BASATA WAMPONGEZA MAYUNGA KWA KUWAKILISHA VYEMA TANZANIA

Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (kulia)akipokea tuzo aliyoipata Nalimi Mayunga mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Afrika. Shughuli hii imefanyika jana katika halfa ya kumpongeza Mayunga kwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars iliyofanyika katika ofisi za BASATA. Akishuhudia kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (Katikati) akiongea katika halfa ya kumpongeza mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo na kuiwakilisha vyema Tanzania . halfa hiyo ilifanyika katika ofisi za BASATA Ilala Dar es Saalam. kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.

Baraza la sanaa Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano ya muziki yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika .

Mwisho mwa mwezi wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha kwenda kushiriki mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya  na kumtakia kila  laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu aliweza kufanya vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Star wa Afrika.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...