Friday, April 17, 2015

WATU 24 WANAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA KUFUATIA AJALI MBAYA YA GARI LA ABIRIA ( HIACE ) ILIYOTOKEA LEO ASUBUHI KIWIRA MKOAINI MBEYA.

"Ajali ya Hiace imeua watu 24 eneo la Uwanja wa ndege Kiwila Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Wadau Niko eneo la tukio, mpaka sasa miili 22 imefanikiwa kutolewa. Kwani Hiace hii ilitumbukia mtoni na bado miili miwili imenasa, ndiyo inatolewa muda huu,

Watu wawili tu ndio wamepona akiwemo kondakta. Ajali hii imetokea wakati Coaster zinazofanya safari zake kati ya Mbeya na Kyela kugoma hivyo baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria. Inaonekana ni ugeni Wa barabara, speed na gari kukosa break za kuaminika.",

Hiyo ni taarifa tuliotumiwa sambamba na picha ndani ya chumba chetu cha habari mapema leo asubuhi kuhusiana na tukio hilo la kusikitisha. 

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.
SOURCE: http://michuzijr.blogspot.com/

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...