Wakazi wa Mloganzila wa Kata ya Kwembe wilayani Kinondoni wakiwa katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili kudai fidia maeneo yalichukuliwa katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kufatilia Madai kwa Wakazi wa Mloganzila –Kwembe,Fedrick Schone akitoa malalamiko yao katika Ofisi za wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angela Kairuki akisikiliza madai ya wananchi wao leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angela Kairuki akizungumza na baadhi ya wananchi katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi juu ya wananchi walioenda kudai fidia za maeneo yalichukuliwa katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAKAZI wa Mloganzila wa Kata ya Kwembe wilayani Kinondoni leo wameandamana katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili kudai fidia maeneo yalichukuliwa katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,jijini Dar es Salaam.
Kuandamana huko kumetokana na serikali kuchelewa kutoa majibu juu ya fidia ya ardhi pamoja na mapunjo ya fidia yaliyotokana na nyumba ,mashamba katika eneo hilo lililochukuwa na mradi huo.
Maandamano yalikuwa ya aina yake kutokana na kuwa na misafara ya magari matatu na kuingia mmoja moja na kisha kujaa katika mlango mkuu wa wizara hiyo na kuanza kupiga kelele kwa kile walichodai hatima yao ya kulipwa ili waendelee na maisha yao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kufatilia Madai kwa Wakazi wa Mloganzila –Kwembe ,Fedrick Schone kufika kwa wanachi katika ofisi ni katokana na kuwepo kwa kalenda nyingi zisisotoa suluhu ya mgogoro wao wa madai.
Amesema kamati yao imekosa kuaminika kutokana na kupeleka majibu ambayo yamekuwa yakiibua maswali mengi kwa wananchi waliochuliwa maeneo yao.
Akizungumza wananchi hao,Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angela Kairuki amesema madai yao watashughulikia ndani ya siku saba kwa kwenda kuzungumza na wananchi hao baada ya kujadili na Waziri wake.
Amesema kuwa suala hilo limefika na kudai anawapa barua juu ya utekelezaji ndani katika kuweza kufikia suluhu na kuwataka kuondoa wasisi wa jambo hilo.
No comments:
Post a Comment