Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.

Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudua NHC na DSE wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudua NHC na DSE wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.
Watendaji wa NHC na DSE wakibadilishana mawazo wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa Tuntufye Mwambusi na Meneja wa Uendelezaji Biashara wa NHC, Willia Genya wakibadiliashana mawazo katika hafla hiyo.
Mchechu akibadilishana mawazo na watendaji wa DSE wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakifuatilia jambo katika hafla hiyo ya utiaji saini.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
Watendaji wa DSE wakibadilishana mawazo wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.
*************************************************************
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI UTIAJI SAINI MANUNUZI YA ENEO LA OFISI KWENYE JENGO LA
MOROCCO SQUARE KATI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) NA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM
Kwa
mara nyingine Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Jumatano, 22 Aprili 2015
tumefikia makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa
kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi
huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.
Mkataba
unaosainiwa leo baina ya pande hizi mbili utagharimu kiasi cha dola za
kimarekani 1,800,000 (bila VAT) kiasi cha shilingi za kitanzania 3.366 bilioni
malipo yatakayofanyika kwa awamu nne katika kipindi cha miaka mitatu.
Mradi
wa kipee na wa kwanza Tanzania wa Morocco Square wenye ukubwa wa mita za mraba
105,000 unaotarajia kukamilika ndani ya kipindi cha Miaka Mitatu, ni
unaotekelezwa kwa kutumia mfumo mpya kabisa wa ujenzi wa (Design and Building).
Umebuniwa kwa makini kabisa kulingana na mahitaji ya majengo ya sasa na ya
baadae na vile vile unajengwa na mkandarasi wa kitanzania. Sambamba na haya,
utekelezaji wa mradi huu umezingatia uwepo wa huduma zote muhimu sambamba na
miundo mbadala yakujitosheleza.
Sifa
nyingine za ziada za mradi huu ni pamoja na uwepo wa majengo pacha mawili
makubwa ya ghorofa, moja likiwa na ghorofa 17 na 19.
Jengo
hili limebiniwa likiwa na mahitaji muhimu yakiwa sehemu moja (Mixed
Development) ikiwepo maeneo maalum ya Maofisi ya kimataifa, Sehemu ya hotel kwa
ajili ya wafanyabiashara, nyumba za makazi (Residential apartment), maeneo ya
maegesho ya magari, huduma za kibenki, pamoja na sehemu ya huduma za masoko (
shopping mall).
Mradi
huu unatarajiwa kuboresha mazingira ya biashara katika jiji la Dar Es Salaam
vile vile ukizingatia mahitaji ya ukuaji na upanukaji wa jiji la Dar Es Salaam.
Jengo la Morocco Square lipo karibu kabisa na kitovu cha jiji likiwa
limezungukwa na maofisi na makazi muhimu kabisa. Eneo la Morocco Square linatoa
fursa kwa mkazi kuweza kufika kwa karibu kabisa sehemu mbalimbali muhimu za
jiji la Dar Es Salaam kama vile Mikocheni, Oystebay, Masaki,Mikocheni, katikati
ya jiji la Dar Es Salaam,Kinondoni, Kawe na Mlimani City.
Makubaliano
haya kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na Soko la Hisa la Dar Es
Salaam ( Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE) yanatoa fursa za kipekee kwa (DSE)
pamoja na mawakala wake wa soko la mitaji na tunapenda kulipongeza soko la hisa
kwa kuwahi kabla ya mashirika yote ili kuweza kupata fursa ya kipekee katika jengo
hili la kisasa kabisa na la kwanza Tanzania.
Tunapenda
kutoa wito kwa Mashirika ya kimataifa, yakati ( Medium Enterprises) kuchanmkia
fursa hii ya kipekee ususani ukizingatia kwamba miji yote Duniani soko la hisa
huwa chachu ya maendeleo ya wadau wote wanaofanya biashara kuzunguka eneo
husika.
Sifa
za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalumu linalowezesha kutua helikopta,
eneo kubwa la maegesho ya magari ya ziada, Ofisi ya Meneja wa Usimamizi wa
Milki, eneo maalumu la kukusanyia taka, nyumba ya mlinzi, umeme wa uhakika,
miundombinu ya zimamoto, mfumo wa vipoza joto, kebo za mtandao wa mawasiliano,
lifti, ulinzi wa saa 24 wa Kamera za CCTV na kisima kirefu cha maji chenye
mfumo wa kusukuma maji ya kutosha.
Tunawahamasisha
wenye kuhitaji maeneo ya ofisi, biashara na nyumba za kuishi wafanye
mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili
ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.
Ukiwa
mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua ofisi au
kuwekeza katika mradi huu, tafadhali wasiliana na Kitengo cha Mauzo, Makao
Makuu ya NHC au piga simu namba 0754 444 333; baruapepe: sales@nhctz.com na pia
tembelea tovuti ya Shirika www.nhctz.com
kwa maelezo zaidi.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA
MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA LA NYUMBA
LA TAIFA
No comments:
Post a Comment