Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari MAELEZO Ajijini Dar es Salaam leo kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa kulia ni Afisa masoko wa NHBRA Zubeda Salum.
Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akionyesha aina ya kwanza ya kigae cha kupaulia nyumba,kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa kulia ni Afisa masoko wa NHBRA Zubeda Salum.
Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akionyesha aina ya pili ya kigae cha kupaulia nyumba,kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa.
Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa kuonyesha aina mbalimbali za vigae vinavyoweza kutengenezwa na kila mwananchi hapa nchini katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)
Na Avila Kakingo,Globu ya Jami.
WAKALA Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wamegundua njia rahisi ya kuboresha makazi kwa kutumia vigae kwa gharama nafuu ambazo kila mwananchi anaweza kuzimudu.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.
Kwemana amesema kuwa utengenezaji wa vigae hivyo ni rahisi na gharama hafuu kwani bidhaa zote za kutengeneza vigae hivyo zinapatikana hapa hapa nchini.
Hifaa hivyo vinavyotumika kutengenezea vigae hivyo ni mchanga sementi na nyuzi za katani bidhaa hizo zote zinapatikana hapahapa nchini, ikiwa kuna mashine inayotumika kushindilia mchanga uliochanganywa na sementi nayo ni gharama nafuu ukilinganisha na faida zinazopatikana.
Kwemana amesema kuwa njia ya kutengeneza vigae hivyo vitasaidia kutumika kama njia nyingine ya kupaua nyumba zetu ambapo vigae hivyo huu kaa muda mrefu kuliko kutumia Nyasi au Bati.
No comments:
Post a Comment