Wajumbe wa kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi wakitembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Idara ya Ujenzi wa Barabara (UUB). Mwenyekiti wa Kamati hiyo wakwanza (kushoto) Mahmoud Muhammed Mussa akiwa na wajumbe wenzake na watendaji wakuu wa UUB wakikagua barabara ya Chaani iliopo Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Mhandisi Mkuu wa UUB Eng. Cosmas Masolwa akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi juu ya ukarabati unaoendelea wa kuihami njia ya Chaani kwa kuwekewa kifusi kabla ya kukamilishwa ujenzi wake kwa kiwango cha lami hap baadae.
Sehemu ya barabara ya Chaani iliyotembelewa na Kamati hiyo ambayo inafanyiwa matengenezo ya kutiwa kifusi ili weze kupitika huku ikisubiri ujenzi wake kwa kiwango cha lami hapo baadae.
No comments:
Post a Comment