Sunday, April 26, 2015

MSHINDI WA PROMOSHENI YA SHIKA NDINGA AKABIDHIWA ZAWADI YAKE


Dennis Ssebo Kutoka kituo cha redio cha EFM akizungumza na mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Sar es salaam Mh. Meck Sadick wakati wa promosheni ya shindano la Shika Ndinga iliyofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe jijini Dar es salaam kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni  Mh. Paul Makonda.
………………………………………………………………….
Hatimaye Washindi washindano la shika ndinga la 93.7 EFM wapatikana baada ya mchuano mkali uliofanyika jana tarehe 25 mwezi wanne katika viwanja vya Tanganyika pakers kawe. Fainali hiyo ilihusisha washiriki kumi kutoka katika wilaya 3za mkoa wa dar-es-salaam kumi tano kati yao wakiwa wanawake na kumi na tano wakiwa ni wanaume.
Shindano hilo lilihudhuriwa na mkuu wa mkoa mheshimiwa Sadiq Mecky Said akiwa kama mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya kinondoni mheshimiwa Paul Makonda na naibu meya wa wilaya ya temeke mheshimiwa Jumma mkenga.
Akiongea jana mheshimiwa Sadiq Said alisema ni ubunifu wa hali ya juu ulioneshwa na kituo cha 93.7 EFM kwa kuanzisha shindano la aina yake ambalo litaongeza ajira kwa vijana na kuinua hali zao za uchumi ,pia aliwahasa washindi kutumia ndinga walizoshinda ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa upande wake mheshimiwa Paul Makonda alisema vijana wajifunze kujitokeza katika mashindano kama haya maana zaidi ya kuburudisha yanabadilisha maisha yao kwa namna yatofauti.
Washindi waliojishindia ndinga kwa upande wa wanaume ni Gabriel Robert kutoka wilaya ya temeke mwenye umri wa miaka 36 na Stella Joseph kutoka wilaya ya ilala mwenye umri wa miak 26 ambao kwa pamoja wamesema shindano halikuwa rahisi na wanafuraha kubwa ya kujishindia gari hizo ambazo watazitumia katika biashara zao aidha wameishukuru redio ya 93.7 EFM kwa kuandaa shindano hilo na kuwashauri wasikilizaji waendelee kusikiliza redio hiyo maana inajali wasikilizaji wake.
SE2SE8

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...