Mkurugenzi Mtendaji wa na taasisi ya utafiti wa vyuo vikuu kusini mwa Afrika (ESAURP), Profesa Ted Maliyamkono akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati unaofanywa kwa kushirikiana na FSDT.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Omari Issa akizindua mradi wa kujengea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati kuhuisha biashara zao ili kupata huduma za kibenki.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Taasisi ya Ukuzaji wa Sekta ya Fedha (FSDT), akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati unaofanywa kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti wa vyuo vikuu kusini mwa Afrika (ESAURP)
wadau wakishuudia uzinduzi huo
……………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Zaidi ya wajasiriamali 1500 inchini watafaidika na mradi wa kujenga uwezo wa kibiashara unaolenga kuimarisha weledi wa kufanya biashara kutoka katika mfumo usio rasimi na kuelekea kufanya shughuli zao katika mfumo rasmi.
Mradi huo unaofadhiliwa na taasisi ya ukuzaji sekta ya fedha nchini (FSDT) na kutekelezwa na program ya utafiti ya vyuo vikuu vya nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAURP) ni mwendelezo wa mradi kama huo uliotekelezwa mwaka 2013 na ESAURP ambapo safari hii unalenga kufikia mikoa kumi ya Arusha, Kilimanajaro, Mbeya, Iringa, Kagera, Mtwara, Kigoma, Singida, Morogoro, Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa ESAURP, Profesa Ted Maliyamkono amesema pamoja na mambo mengine mradi unalenga kusaidia biashara ndogo na za kati zinazoendeshwa katika mfumo usio rasimi kupata uwezo na maarifa ya kusaidia kukua na kuwa sekta rasimi, kupata huduma za kifedha, pia kufahamu benki washirika ili kutengeneza mabadiliko ya tamaduni za kibenki namna ya kusaidia miradi ya sekta isiyo rasimi katika miradi inayotafuta huduma za kibenki hasa mikopo.
“Lengo kuu la mradi ni kujenga uwezo wa biashara ndogo na za kati zaidi ya 1500 kukua. Jambo ambalo litafanyika kwa kutengeneza program ya mafunzo inayolenga kusaidia biashara ndogo kushiriki katika uchumi rasmi” alisema Profesa Maliyamkono.
Mradi pia utatengeneza kada ya wakufunzi wenye uzoefu ambao watatoa mafunzo ya kukuza ujuzi wa kibiashara kwa biashara ndogondogo nchi nzima hivyo kuongeza idadi ya huduma za kibiashara nchini na kupanua uwezo wa maendeleo ya kibiashara nchini.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Ufundi wa wa FSDT, Sosthenes Kewe aliwaambia waandishi wa habari kuwa, taasisi yake imesaidia mradi huu kwa kuwa unaendana na kazi yao ya kuwezesha wajasiriamali wadogo na wakati na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi, kutengeneza ajira na kupanua vyanzo vya kodi.
“Biashara ndogondogo na za kati zinanaendelea kutambulika kama vichocheo muhimu kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo katika nchi za Afrika. Kama wachangiaji wa pato la vizazi na ajira, kwa hiyo zina nafasi maalumu ya kukuza sekta binafsi” alisema bwana Omari Issa, Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa.
Mradi huo unahusisha kujenga mazingira ya kurasimisha biashara na program ya kujenga uwezo kwa kufanya mafunzo ya siku 5 kwa wajasiriamali watakaochaguliwa kila mkoa na mafunzo yatakayolenga
• Usimamizi wa biashara,
• Usimamizi wa fedha,
• Kutunza kumbukumbu,
• Kusajiri biashara,
• Masuala ya kodi nk
Mafunzo hayo yatafuatiwa na usimamizi kwa miezi mitatu (ulezi)na kuandaa vituo vya usaidizi wa kibiashara ambavyo vitafanya kazi kwa miezi mitatu kwenye mikoa husika.
Mradi huu ni umeanzishwa kwa pamoja FSDT, ESAURP na taasisi shiriki za kifedha nchini.

No comments:
Post a Comment