Tuesday, April 28, 2015

UWAWATA WAMKABIDHI WAZIRI CHIKAWE RIPOTI INAYOPINGA UPIGAJI WA RAMLI NA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE NCHINI

 Mratibu Mkuu wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania (Uwawata), Julius Juju (wapili kulia) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, ripoti inayopinga upigaji wa ramli na mauaji ya albino na vikongwe nchini. Ripoti hiyo iliyoandaliwa na zaidi ya Wajumbe 200 wa Uwawata baada ya kufanya utafiti ya mauaji ya albino katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kufanya semina ya hitimisho jijini Mwanza kwa kutoa maazimio ya kupinga mauaji hayo. Kulia ni Mkaguzi wa Waganga nchini katika umoja huo, Mohamed Masoud, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Uwawata Mkoa wa Dar es Salaam, Swed Omari. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.    
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akiionyesha ripoti inayopinga upigaji wa ramli na mauaji ya albino na vikongwe nchini mara baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo na Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania (Uwawata), ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Ripoti hiyo iliandaliwa na zaidi ya Wajumbe 200 wa Uwawata baada ya kufanya utafiti ya mauaji ya albino katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kufanya semina ya hitimisho jijini Mwanza kwa kutoa maazimio ya kupinga mauaji hayo. Kulia ni Mkaguzi wa Waganga nchini katika umoja huo, Mohamed Masoud, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Uwawata Mkoa wa Dar es Salaam, Swed Omari, na wapili kulia ni Mratibu Mkuu wa Uwawata nchini, Julius Juju.  Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiwashukuru viongozi wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili nchini (Uwawata), kwa kumkabidhi ripoti inayopinga upigaji wa ramli na mauaji ya albino na vikongwe nchini, ofisini kwa Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo. Ripoti hiyo iliandaliwa na zaidi ya Wajumbe 200 wa Uwawata baada ya kufanya utafiti ya mauaji ya albino katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kufanya semina ya hitimisho jijini Mwanza kwa kutoa maazimio ya kupinga mauaji hayo. Wapili kulia ni Mratibu Mkuu wa Uwawata nchini, Julius Juju na Kulia ni Mkaguzi wa Waganga nchini katika umoja huo, Mohamed Masoud. 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...