Wednesday, April 15, 2015

BALOZI WA UINGEREZA AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimkaribisha ofisini kwake, Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose, wakati balozi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadiliana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania.
 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.  Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.  

No comments:

TANAPA YAMPONGEZA SIMBU; YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAE KUTANGAZA HIFADHI ZA TAIFA KUPITIA MCHEZO WA RIADHA

Na. Philipo Hassan, Arusha Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, CPA Musa Nassoro Kuji, amempongeza rasmi Sajini Taji Alphonce Simbu, bingwa wa D...