Wednesday, April 02, 2014

NHC Kilimanjaro yatoa msaada wa bati kwa wahanga wa mvua ya Upepo wilaya za Mwanga na Hai


Meneja wa shirika la nyumba la taifa mkoa wa Kilimanjaro Shehe Kombo akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa bati kwa wahanga wa mvua iliyoambatana na Upepo mkali katika wilaya za Hai na Mwanga.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza kabla ya kukabidhiwa msaada wa bati kwa wahanga wa mvua iliyoambatana na Upepo mkali katika wilaya za Hai na Mwanga.
Watumishi wa shirika la nyumba la taifa NHC mkoa wa Kilimanjaro
Msaada wa bati ukishushwa .
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akipokea msaada wa bati toka kwa meneja wa shirika la nyumba la taifa NHC mkoa wa Kilimanjaro Shehe Kombo kama msaada kwa wahanga wa mvua iliyoambatana na Upepo mkali katika wilaya za Hai na Mwanga.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkabidhi msaada wa bati zilizotolewa na shirika la nyumba la taifa NHC mkoa wa Kilimanjaro, mkuu wa wilaya ya Hai,Noavatus Makunga .
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkabidhi msaada wa bati zilizotolewa na shirika la nyumba la taifa NHC mkoa wa Kilimanjaro, mkuu wa wilaya ya Mwanga,Shahib Ndemanga.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimshukuru Meneja wa shirika la nyumba la taifa NHC mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kukabidhiwa msaada wa bati kwa ajili ya wahanga  wa mvua iliyoambatana na Upepo mkali katika wilaya za Hai na Mwanga.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa NHC mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wakuu wa wilaya waliopatiwa msaada wa bati.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...