Monday, February 18, 2008

Ziara ya Bush

Dinner Ikulu jana..











Shughuli ya utiaji saini Ikulu asubuhi


Hahaahahahaaaa ndivyo wanavyoonekana wanajeshi hawa wawili wa zamani wakicheka kwa pamoja.
Jamaaa kafuraaaahi kinoma huenda hakuwahi kupata generosity ya aina hii ya watu kuacha kazi na kisha kumpokea yeyetu.
Hii furaha ya hawa Marais inaashiria mambo fulani makubwa ambayo bila shaka hatuyajui na hatutayajua mpaka yatakapofunuliwa, haiwezekani Marekani ikawa rafiki ghafla, hawanarafiki hawa jamaa anyway we just wait and see.


Kama vile anamuambia ebwaana mambo vipi, unaonekana uko fiti Kanali, mwenzio mimi nilikimbia jeshi kule Marekani, vipi wwewe unaendelea.

Makamanda wawili wa jeshi wakiwa wanatoa speech hawa jamaa, nadhani wanapatana sababu ya ujeshi, nani kamanda mkubwa kuliko mwingine kati yao.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi Condoreza Rice akiwasalimia wananchi alipoingia Ikulu Dar jana. Alikuwa na mvuto wa kipekee sijui kwakuwa ni bomba ama kw akuw ani black?

Askari wa Marekani akipita na mbwa ili kuhakikisha kuwa maeneo hayo ni salama kwa wazee kuingia.


Mama Bush na mama Kikwete


Pichaa za juu ni Rais George Bush wa Marekani wakitia saini msaada mkubwa wa $ 700 Million kutoka serikali ya Marekani , Mkataba huo umekusudia kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa barabara tatu ambazo ni barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga,Tunduru Songea hadi Mbambabay na barabara ya Horohoro hadi Tanga na pia msaada huo mradi wa umeme katika mkoa wa Kigoma, mara baada ya kutia saini mlataba huo Rais Bush na Rais Kikwete walitembelea hospitali ya Amana iliyopo wilayani Ilala imepata mafanikio makubwa katika mradi wa mapambano dhidi ya Ukimwi ambapo pia umedhaminiwa na serikali ya Marekani.
 
Rais Bush anatarajia kwenda mkoani Arusha na kufanya shughuli ambako atalala na kurejea Dar es Salaam siku inayofuata na kuhitimisha Ziara yake nchini Tanzania na kuelekea Kigali nchini Rwanda.
(Picha Mpoki Bukuku na Reuters)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...