Monday, February 25, 2008

Matokeo rasmi ya uchaguzi wa Kiteto

HABARI zilizotufikia hvi punde zinaeleza kwamba Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kiteto, Benedict Nangoro ameibuka mshindi baada ya kuzoa kura nyingi katika uchaguzi ulofanyika juzi na kura kuanza kuhesabiwa juzi hiyo hiyo hadi jana mchana.

Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo jana jioni, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Festo Kang'ombe alisema kuwa Nangoro ambaye ni mgombea wa CCM ameibuka mshindi kwa kupata kura 21,506, wakati mgombea wa Chadema, Victor Kimesera alipata kura 12,561, mgombea wa Sauti ya Umma (Sau) Mashaka Fundi alipata kura 300 na mgombea wa PPT-Maendeleo, Juma Saini aliambulia kura 110.





Kang'ombe alisema kwamba idadi ya watu waliojiandikisha ni 74, 626, lakini waliokwenda kupiga kura ni 35, 261, idadi ambayo karibu ya nusu hawakwenda kupiga kura.

Hawa jamaa hawakuamini kabisa nini kimetokea (Picha zote za Mpoki Bukuku)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...