Friday, February 08, 2008

Waziri Mkuu mpya Mizengo Pinda


Kikao cha bunge kimeanza tena jionni hii mjini dodoma na jina limeshaletwa la Waziri Mkuu mteule. Jina hilo ni Mizengo Kayanza Peter Pinda na sasa tunasubiri wabunge wapige kura, hivi sasa wabunge wanaunga mkono hoja kaanza Hamad Rashid Mohammed kasifia saana akafuata Edward Lowassa naye kasifia ile mbaya, akafuata mama Getrude Mongela amesifu mpaka sijui vipi.

Sasa wanazungumza Anna Abdallah, Zitto Kabwe, John Malechela, Jackson Makwetta na wengineo. Ni mizengo Pinda waziri mkuu mpya!!!!. Picha ni ya mdau Edwin Mjwahuzi aliyepo Dodoma.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...