Saturday, February 16, 2008

Mtoto adondoka kutoka kwenye ungo


MTOTO mwenye umri wa miaka 12 (katikati) mkazi wa kijiji cha Kilima Hewa mkoani Mtwara amekutwa akiwa uchi kwenye eneo la Kanisa la Kristo Mfalme, Tabata jijini Dar es salaam baada ya kuanguka kutoka kwenye ungo waliokuwa wakisafiria kishirikina.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, mtoto huyo alisema yeye na bibi yake, Binti Abdala Mkumba walikuwa wakisafiri kutoka Mtwara kwa usafiri wa ungo wakielekea mjini Morogoro kwenye mkutano.

Alisema safari hiyo ambayo ilijumuisha wachawi wapatao 50 ilikuwa na lengo la kumpokea mshirikina mwenzao aliyejiunga katika kundi lao nchini hivi karibuni ili kumjengea nguvu na uwezo wa kupambana na nguvu nyingine.

“Tukiwa njiani nilimwambia bibi endesha vizuri ungo na usipite katika maeneo ya kanisa yeye hakunisikia, baada ya muda mfupi tulipofika katika kanisa la Kristo Mfalme ndipo ungo ulitikiswa na nguvu na mimi nikaanguka chini, ” alisema mtoto huyo.

Msaidizi wa Paroko wa Kanisa hilo, Padri Claudi Kambini aliyeambatana na mtoto huyo hadi ofisi za Mwananchi, alisema tukio hilo lilitokea jana ya saa tatu usiku. (Stori imendikwa na Peter Edson)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...