Monday, February 11, 2008

Kikwete aahirisha kutangaza baraza la mawaziri

Taarifa tulizo nazo hadi sasa ni kwamba Rais Jakaya Kikwete atatangaza baraza la mawaziri kesho saa nne asubuhi, badala ya leo kutokana na sababu mbalimbali, hali iinayofanya kuwepo kwa hali ya tension kubwa kwa jamii.

Taarifa zisizo rasmi ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa kuahirishwa huko kunatokana na Rais Kikwete kuteua baadhi ya mawaziri kutoka ndani ya chama ambao baadhi wamedaiwa kukataa nyadhifa.

Hata hivyo uvumi mwingine uliokuwa umeenea jana kiasi cha kusababisha tafrani miongoni mwa baadhi ya wananchi na hata wanachama wa vyama vya upinzani na hata CCm ni zille zilizodai kuwa Rais aliteua mawaziri wanne kutoka kambi ya upinzani, ambao walikuwa wapewe nyadhifa katika wizara nyeti.

Lakini taarifa zilizopatikana baadaye zilipingana na taarifa hizo na hakuna hata mmoja aliyethibitisha si viongozi wa vyama vya upinzani na hata wale wa chama cha mapinduzi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...