Saturday, February 16, 2008

Bush Katua Tanzania

Rais Bush katua bongo kiasi cha dakika 40 zilizopita, kapigiwa mizinga 21 na amepita kukagua gwaride la heshima na wakati akikagua gwaride la heshima huyu bwana kafurahisha kitu kimoja alikuwa akitembea na kuact kama mwenyeji kwani mara kadhaa alionekana kumuongoza Rais Kikwete namna ya kutembea na mara kadhaa alimuintercept, kisha akasalimiana na mawaziri wa bongo.

Waziri aliyefurahisa kupita wote ni Waziri wa Maliasili na Utalii bi Shamsa Mwangunga kwani mara baada ya kusalimiwa na Bush na kuzungumza kwa sekunde kadhaa akawa kama aliyepumbaa kidogo aliwapita mawaziri wengine wote na akaenda mbele lakini baadaye akarudi na kuendelea na salamu.

Kwa kweli mji umeng'ara si mchezo barabara zinapigga deki na zimepambwa na bendera kibao za Marekani. Picha zote za Reuters


Akisalimiana na mmoja wa waliofika kumlaki
Akikagua gwaride
Akiteta jambo na Bush



No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...