Friday, February 08, 2008

Hosea naye chali


Taarifa zilizopatikana mjini Dodoma sasa hivi ingawa hazijathibitishwa zinasema kwamba Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Dk, Edward Hosea naye amejiuzulu. Taarifa hizo zinasema Mkurugenzi huyo alijiuzulu rasmi jana usiku na anasubiri ridhaa ya Rais.

Huyu anakuwa mtu wa nne kujiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond kampuni ya mkobani iliyolisababishia taifa hasara ya mamilioni. Taarifa zaidi vipande vipande tutakuwa tukiwaletea kadri muda unavyosonga mbele.

Pia hivi sasa Dr Mwakyembe ambaye ni Mwenyekiti wa Tume iliyoibua madudu ya Richmond hivi sasa analindwa na boarguard.


Taarifa tulizozipata sasa zinasema kuwa JK amekubali ombi la kujiuzulu la Dk Edward Hosea (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru kuanzia saa 6.00 mchana leo. Anayekaimu ofisi hiyo nyeti, ni aliyekuwa naibu wake, Lilian Mashaka. Takukuru imetajwa kwa kuwalinda watuhumiwa wa ufisadi katika kashfa ya Richmond.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...