Tuesday, February 05, 2008

Baraza lawachukulia hatua waliofanya operesheni tatawaliofanya operesheni tata

BARAZA la Madaktari nchini (MCT) limewaandikia barua za kujieleza madaktari sita wanaotuhumiwa kwa upasuaji wa wagonjwa wawili waliopasuliwa kinyume na magonjwa yao, katika Taasisi ya Tiba ya Mifuta Muhimbili (MOI) Novemba mosi mwaka jana.

Wagonjwa hao ni Emmanuel Didas (19) aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya goti na bado amelazwa MOI kwa matibabu zaidi, mwingine ni Emmanuel Mgaya (20) aliyefanyiwa upasuaji wa goti badala ya kichwa na hivi sasa ni marehemu.

Akizungumzaa Mwandishi wa habari hii jana kwa njia ya siku yake ya kiganjani Msajili wa MCT Palloti Luena alisema kwamba baraza hilo limeshaanza hatua za awali kuhusu suala la watuhumiwa hao.

Luena alisema kwamba hatua walizoanzia ni kuwaandikia barua watuhumiwa ili wajieleze kwanza kwajia ya maandishi na baada ya hapo wataitwa rasmi katika baraza hilo kwa ajili ya kujibu tuhuma zao.

“Tumewaandikia barua za kujieleza na baada ya wao kurejesha majibu, ndipo tutawaita rasmi katika baraza ili wajibu tuhuma zao,”alisema Luena.

Luena alifafanua kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa baraza hilo kabla kesi hazijasikilizwa watuhumiwa wanaandikiwa barua na wanapewa muda wa wiki mbili kujibu mabarua hizo, ndipo wanaitwa katika baraza kujibu tuhuma zinazo wakabili.

Desemba 21, mwaka jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa alitangaza ripoti ya tume aliyoiunda kuchunguza utata wa upasuaji wa wagonjwa MOI na kueleza kuwa utata huo ulisababishwa na uzembe uliofanywa na madakatari katika hospitali hiyo.

Mwakyusa alisema madaktari wawili bingwa, watatu wa ngazi ya chini na daktari mmoja wa dawa za usingizi , watafikishwa katika baraza hilo kujibu tuhuma za uzembe huo.

Mwakyusa alisema hayo wakati akisoma ripoti ya tume aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza tukio la upasuaji tata wa wagonjwa hao, ambapo alisisitiza kwamba kitaaluma hairuhusiwi kuwataja majina madaktari hao mpaka baraza husika itakapotoa hukumu. Taarifa hii ya Jackson Odoyo

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...