Thursday, February 14, 2008

Rais Kikwete akutana na Wazee Dar


Rais Kikwete amemaliza kuzungumza na wazee wa jiji la Dar es Salaam amezungumza meengi sana, lakini kwa uchache naweza kuwadokoleeni ni kwamba ameelezea kilichomfanya abomoe baraza la mawaziri na kwamba akasisitiza kulikuwa hakuna namna, bali ilikuwa ni lazima waziri mkuu wake ang'oke kwa sababu lukuki.

Mosi upepo mbaya uliovuma dhidi ya serikali yake,
Pili, maoni ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali,
tatu, hali ilikuwa mbaya hivyo haikuwa rahisi kumchekea.
Kwa mantiki hiyo ilikuwa ni lazima jamaa ang'oke na si kwamba alijiuzulu kwa tafsiri ya haraka haraka. Kingine ni kwamba anasubiri mapendekezo ya bunge ili kusudi aangalie nini cha kufanya. Pia kazungumzia ujio wa Joji Kichaka wa Marikani akaomba kuwapo mapokezi ya kina.
Lakini katika yooote wazee wameboa ile mbaya, wametoa speech laini mno ambayo hawakustahili kuitoa wao, yaani ni kama vile wanaogopa kitu fulani, wakati tulitarajia wao ndiyo wangemsaidia kukemea, kinyume chake wamezungumza mambo ya jumla mno. Picha ya Faraja Jube.

1 comment:

Anonymous said...

Wazee tena wanamwogopa mtoto wao...!Hii haijatulia kabisa .. waliatakiwa wapige pini nzito kuhusu mafiasdi wanaotumaliza sisi wajukuu...

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...