Thursday, February 07, 2008

Ndesa, Dr Slaa, Mama malechela wamwaga sumu

Baada ya Dk Msabaha kuketi Spika amempa ukumbi Mama Anna Kilango ambaye ndiyo anachangia sasa, akianza kusoma vifungu vya sheria vya katiba, kiufupi ameua na hajaogopa kitu amemwaga mboga na ugali ili wakose wote kama mnakumbuka huyu mama ndo angekuwa first lady.

Hajaacha lolote kampaka Lowassa matope ile mbaya na kiasi akafikia akasema liwalo na liwe, nabidi uanzwe mwanzo mpya, ameponda sana kauli ya Waziri Mkuu kusema ameonewa.

Amesema ushahidi ni mwingi kwamba richmond ni kampuni tapeli na anadai ana uhakika baraza zima la mawaziri linajua hilo na kwamba kampuni hiyo ilipewa tenda wakati haijasajiliwa.

Dk Slaa akasoma vifungu kisha naye akamwaga sumu nyingi tuu akisema waziri mkuu na baraza lake lote wawajibike kwa kushindwa kusimamia shughuli zake kuhusiana na zabuni.

Ametaka pia tanesco ipongezwe kwa kuiarifu serikali kwamba zabuni imekwenda kinyume lakini barua zake zote hazikujibiwa. uwajibikaji ni mawaziri na makatibu wakuu wa wizara husika zote.

Mbunge bunge wa moshi Ndesamburo ameomba mwanasheria mkuu na mkurugenzi wa takukuru wawajibishwe pia, na kwamba hili ni dili limefanyika na ameomba hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika wote.

Amesema madhambi yaliyofanyika ndiyo yaliyochangia kupanda kwa bei ya umeme na lazima kitu kifanyike, na kiongozi yeyote mwenye madhambi na ana kimrija kwenye dili hilo awajibike. ametaka hatua za kisheria zichukuliwe na wahusika kufilisiwa.

Mbunge wa Kasulu Magharibi , Kilontsi Mporogomyi ambaye pia ni fisadi mstaafu, amemwaga sumu akitaka uwepo mwanzo mpya kwa kila mtu kuwajibika na lake akasema huu si wakati wa kuogopana. Ameitaja wazi wazi Richmond ni kampuni ya kitapeli akirejea kuitaja mwaka 2004 na akapuuzwa.

Stanley Kevela Yono yeye pamoja na mengi anataka mafisadi wanyongwe na kisha kushughulikiwa ipasavyo, akitumia utani mwingi tu. Tutaendelea kesho.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...