Monday, February 25, 2008

CCM yanyakua Kiteto

Matokeo ya awali ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kiteto mkoani Manyarayanaonyesha kuwa mgombea bunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Benedict Ole Nangoro ameshinda.

Habari za uhakika zilizokusanywa na gazeti la Tanzania Daima jana usiku baada ya kura kuhesabiwa katika kata zote 15 (ukiacha maeneo machache ambayo alikuwa hajakamilika) yalikuwa yakionyesha kuwa, Nangoro alikuwa amevuna takribani kura 15,000 dhidi ya 11,000 alizokuwa amepata mshindani wake mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera.

Habari zaidi ambazo Tanzania Daima ilikuwa imezipata majira ya saa 5:00 usiku wa kuamkia leo zilikuwav zikionyesha kuwa Nangoro alikuwa ameshinda katika takribani kata 11 kati ya kata zote 15 zilizokwishakusabiwa huku mpinzani wake akishinda katika kata nne tu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...