Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa (mbele) akiongoza kikao cha uzinduzi wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Prof James Mdoe, akielezea historia ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Madini la Taifa (Stamico) limetakiwa kushirikiria uchumi wa nchi kutokana na ubia uliopo kati ya Wabia na Serikali.
Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa, Justin Ntalikwa wakati wa uzinduzi bodi mpya ya Stamico , amesema kuwa mashirika mengi ya serikali yanayosimamia madini ndiyo yamekuwa yakishikiria uchumi wa nchi.
Amesema bodi inawajibu kuhakikisha stamico inabadilika kutokana na miradi iliyo chini yake inaendelezwa na kusimamiwa ipasavyo ili kuipatia serikali manufaa mbalimbali ikiwemo gawio katika migodi ya ubia.
Profesa Ntalikwa amesema kuwa bodi katika kufanya kazi zake moja ni kufanya usaili wa wafanyakazi kutokana nafasi nyingi ikiwemo ya mkurugenzi mtendaji kukaimiwa na zingine.
Aidha amesema kuwa ina wajibu wa kuboresha mikataba iliyopo kwa kukaa na wabia ili pande zote ziweze kunufaika na manufaa yatokanayo na miradi ya uwekezaji katika sekta ya madini.
Bodi hiyo iliyoteuliwa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo inaundwa na wajumbe watano ambao ni pamoja na Abdalah Mussa, Dkt. Coretha Komba, Felix Maagi, Dkt. Lightness Mnzava, John Seka chini ya Mwenyekiti wake Balozi Alexander Muganda
No comments:
Post a Comment