Tuesday, December 01, 2015

PINDA AKABIDHI RASMI OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MAJALIWA

pi1Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkaribisha  Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda  ambaye Novemba 30,2015 alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kukabidhi Ofisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi2Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo  Pinda ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015 kukabidhi Ofisi , (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi3Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda wakimsikiliza  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florence Turuka aliposoma taarifa kabla ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi Ofisi, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi4Waziri Mkuu, Mstaafu Mizengo Pinda  akizungumza  kabla ya kukabidhi Ofisi kwa  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa,  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi5Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa  akipokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuujijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
pi6Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka  Kikula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi7Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 215. Watatu Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka  Kikula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pi8Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akifurahia  katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda  na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florence Turuka baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi rasmi Ofisi ya Waziri  kwa  Waziri  Mkuu Majliwa , kwenye ukumbi wa Ofisiya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU mstaafu Mizengo Pinda amekabidhi ofisi kwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na kumtaka aimarishe ufuatiliaji wa maelekezo anayoyatoa kwenda ngazi za chini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika jana jioni (Jumatatu, Novemba 30, 2015), kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam, Bw. Pinda alisema katika kipindi cha uongozi wake kulikuwa na ucheleweshaji wa kupata majibu kutoka ngazi ya chini katika maelekezo aliyokuwa akitoa.
“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na ina mambo mengi ya kufuatilia. Kama kuna changamoto nilikumbana nayo ni ucheleweshaji wa majibu kutokana na maagizo niliyokuwa nikitoa. Itabidi uwe makini sana katika kufuatilia hili,” alisema Waziri Mkuu mstaafu.
Alimtaka ahakikishe kila idara inakuwa na mpango kazi na kunakuwa na ufuatiliaji wa kila kilichopangwa. “Pia ninashauri uandaliwe kikao na watu wa Hazina ili wakueleze jinsi bajeti ya Serikali inavyoandaliwa ili iwe rahisi kwako kufuatilia vipengele kadhaa vya bajeti ya Serikali pindi maswali yanapoulizwa bungeni,” alisema.
Pia alimkabidhi taarifa yenye kurasa 104 ambayo inaelezea majukumu mbalimbali ya taasisi na idara zilizo chini ya Ofisi wa Waziri Mkuu. Ofisi ya Waziri Mkuu ina taasisi nane, idara nane na vitengo saba. Taasisi hizo ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Tume ya Kuratibu na Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Tume ya Uchaguzi (NEC) na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA). Nyingine ni Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Idara zilizopo kwenye ofisi hiyo ni Utawala na Rasimali watu, Sera na Mipango, Uratibu wa Maadhimisho ya Kitaifa na Sekta binafsi na Uwezeshaji. Nyingine ni Bunge na Siasa, uatibu wa shughuli za Serikali, Mpigachapa Mkuu wa Serikali na Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu.
Alisema pia ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi ambayo Rais Dk. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wameanza nayo na kwamba ana imani kwa uchapakazi wao na uadilifu wao,  anaamini wataweza kuivusha Tanzania na kuifikisha kwenye uchumi wa kati ambako Serikali imejielekeza kufika.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimshukuru Waziri Mkuu mstaafu na kumuahidi kutekeleza yote yaliyomo kwenye taarifa aliyomkabidhi. Pia aliahidi kusimamia kwa karibu suala la ufuatiliaji wa maelekezo anayotoa pamoja na yale yanayotoka ngazi za juu.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu, Dk. Florens Turuka, Naibu Katibu Mkuu (OWM), Bibi Regina Kikuli, wakuu wa taasisi zote nane, wakuu wa idara na vitengo vya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wasaidizi wa Waziri Mkuu walioko ofisi yake binafsi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...