Tuesday, September 01, 2015

MAKARANI WA MAHAKAMA MKOA WA DAR ES SALAAM WAPEWA MAFUNZO YA UINGIZAJI WA TAARIFA ZA MASHAURI KWA NJIA YA KI-ELECTRONIKI


 Mshiriki wa mafunzo elekezi juu ya uingizaji wa takwimu za mashauri kwa njia ya kielectroniki (Judicial Stastical Dashboard System JSDS) kwa Makarani wa Mahakama Mkoa wa Dar Es Salaam, Bi. Tumaini Mwalioga akisisitiza neno wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika chuo cha LearnIt leo Jijini Dar Es Salaam.
 Mgeni rasmi Mhe. Solanus Nyimbi (aliyesimama mbele) akitoa nasaha kwa niaba ya Mtendaji Mkuu Mahakama kwa washiriki wa mafunzo maalum ya uingizaji wa takwimu za mashauri kwa njia ya kielectroniki kwa Makarani wa Mahakama Mkoa wa Dar Es Saalaam yanayofanyika katika chuo cha LearnIt Jijini Dar Es Salaam. Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha Makarani waweze kufungua mashauri na kuyaingiza kwa njia ya kiielectroniki. Mpaka sasa mafunzo hayo tayari yameshatolewa kwa jumla ya Makarani 860. Kwa upande wa Dar es Salaam mafunzo haya yatatolewa kwa jumla ya Makarani 90.
Kiongozi wa darasa akisoma risala fupi mbele ya mgeni rasmi kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
 Mgeni rasmi katika mafunzo maalum ya mfumo wa kuingiza taarifa ya mashauri (Judicial Stastical Dashboard System (JSDS)  Mhe.Solanus Nyimbi (walioketi katikati)  Mhe. Mustapha Sihani, Naibu Msajili Mwandamizi Kanda Kuu Dar es Salaam, Patricia Ngunguru, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mafunzo,  Mhe. Said Mkasiwa, Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ilala, (kushoto) ni kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...