Mambo ya Tigo hayooo





TIGO YAENDELEA KUGUSWA NA JAMII PAMOJA NA KUCHANGIA MICHEZO ZANZIBAR

Rais Abeid Aman Karume amevunja ukimwa kuhusu tatizo la umeme na kuhakikishia wananchi kuwa huduma hiyo itarejea katika hali yake ya kawaida kama ilivyokuwa hapo awali

Rais ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki muda mfupi tu baada ya kuelezwa kuwa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imeanzisha huduma ya kusambaza maji kwa wananchi kila mtaa takribani siku kumi zilizopita.

Maji hayo hugawiwa Katika maeneo mbali mbali kwa lengo la kukabiliana na ukosefu wa huduma ya maji kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu

Rais Karume alisema“Tunawapongeza Tigo ka kuamua kuwasaidia na kuwasambazia maji wananchi katika maeneo mbalimbali na kila mmoja wetu anaelewa kwamba unapomsaidia mtu tatizo la maji basi thawabu zake kwa mungu ni nyingi”

Pia katika harakati za kuinua sekta ya michezo Rais wa zanzibar Abied Aman Karume aliisifu kampuni ya simu za mkononi Tigo kwa kudhamini mashindano ya mpira wa kikapu ya Karume Cup kwa mfululizo wa miaka miwili

pamoja na hilo pia Rais alitoa kauli ya kufufua matumaini ya mchezo huo baada ya kuahidi kuwa serikali yake itajenga uwanja wa kisasa wa ndani ili utumike kwa michezo ya kitaifa na kimaifa

Rais alitoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia wanamichezo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa fainali ya kombe la karume mwishoni mwa wiki ambapo Timu ya polisi ilifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichabanga Timu ya Stone town point 67 kwa 42 katika mchezo ulifanyika katika viwaja vya Ghykhana mjini Zanzibar

Nae Meneja Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando akiongelea kujitolea kwa kampuni yake kuhusu tatizo la maji alisema “ukosefu wa maji katika makazi ya wananchi umepelekea sisi Tigo kuguswa na kaumua kusaidia tatizo hili kwa kutambua umuhimu wa maji katika maisha ya binadamu kila siku

Comments

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri