BREKING NYUUUUUUZZZZZ:NEHEMIA MCHECHU AULA NATIONAL HOUSING
Nehemia Kyando Mchechu- Bosi Mkuu Shirika la Nyumba Tanzania [NHC]
Kwa mujibu wa kifungu Na. 18 (1) cha Sheria Na. 2 ya 1990, iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (The National Housing Corporation Act No. 2 of 1990) Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amemteua Ndugu Nehemia Mchechu (37) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Uteuzi huu unaanzia tarehe 1/3/2010.
Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nehemia Mchechu alikuwa Mkurugenzi
Mkuu (Chief Executive Officer) wa Benki ya “Commercial Bank of Africa”.
Chini ya Uongozi wake benki hiyo imepata mafanikio makubwa sana hapa nchini, na ni moja kati ya benki tano zilizoanza utaratibu wa kutoa mikopo ya nyumba kwa Watanzania.
Ndugu Nehemia Mchechu akishirikiana na Bodi mpya ya Shirika hili na timu ya Menejimenti ya Shirika hili, amepewa jukumu la kulifanyia mageuzi makubwa Shirika hili ili liingie katika biashara kubwa ya kujenga nyumba katika Mikoa yote na kuziuza kwa mikopo kwa watanzania wa kipato cha chini na kati, ambalo ndilo lengo kuu la Shirika hili tangu lilipoanzishwa mara tu baada ya Tanganyika kupata Uhuru Desemba 9, 1961.
Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria Na. 2 ya 1990 iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Bwana K. Masudi Issa Msita kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo. Bwana K. Masudi Issa Msita ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi (National Construction Council).
Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria hiyo hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo.
1. Msajili wa Hazina - (Wizara ya Fedha).
2. Mkurugenzi wa Nyumba - (Wizara ya Ardhi).
3. Prof. W.J. Kombe - (Chuo Kikuu cha Ardhi).
4. Bwana Enock Maganga - (Benki Kuu).
5. Bi Subira Mchumo - (Sekta Binafsi).
6. Bwana Elius Mwakalinga - (Wizara ya Miundombinu).
7. Bi. Shally Raymond - (Mbunge)
Uteuzi huu unaanza tarehe 28/02/2010 na ni wa miaka mitatu.
Imetolewa na:-
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi
Comments