Mabalozi wapya: Mwanaidi Majaar - Marekani


Katika taarifa yake ya leo ya redio, TBC1 inatangaza kuwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amemteua balozi Mwanaidi Sinare-Maajar kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani kuchukua nafasi ya balozi Ombeni Sefue.

Balozi huyo anakuwa mwanamke wa kwanza wa Tanzania kushika nafasi hiyo ya ubalozi nchini Marekani. Kabla ya hapo, balozi Majaar alikuwa akishikilia wadhifa kama huo huko nchini Uingereza.

Taarifa hiyo pia inasema kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Afrika Kusini ni bi Radhia Mtengeti-Msuya na anaishika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa balozi katika nafasi hiyo, Emanuel Mwambulukutu, kustaafu.
SOURCE: http://haki-hakingowi.blogspot.com/

Comments

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri