Meli yaungua moto Zenji
Meli ya MV Serengeti ikiungua moto ikiwa iko nje kidogo ya bandari ya Zanzibar, huku wafanyakazi wa shirika la bandari Zanzibar kwa kushirikiana na kikosi cha zimamoto na uokozi (KZU) wakiwa katika jitihada za kuuzima moto huo. Meli hiyo yenye namba za usajili IMO:6818796 ilikua katika matayarisho ya kwenda kisiwani Pemba usiku wa jana, hata hivyo chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika. Picha nyingine wananchi mbalimbali wakishuhudia meli ya MV Serengeti ikiungua moto nje kidogo ya bandari ya Zanzibar.
Comments