Hatima ya Liyumba April





MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Aprili 8, mwaka huu itatoa uamuzi kama washtakiwa watano wanaodaiwa kuchota fedha za EPA, Sh 6 bilioni wana kesi ya kujibu.
Hakimu Sekela Moshi, anayeongoza jopo la mahakimi watatu wanaosikiliza kesi hiyo, alisema hayo mara baada ya upande wa mashaka kuwasilisha majumuisho ya hoja za mwisho ili kuishawishi mahakama kuwaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu au la.
Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Bahati Mahenge, Manase Mwakale, Davies Kamungu, Godfrey Mosha na Eddah Mwakale.

Kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya mwaka 2003 na 2005 walikula njama kuiibia BoT, Sh 6,041,899,876.45 baada ya kudanganya kuwa kampuni yao ya imepewa deni na kampuni ya Marubeni ya nchini Japan.

Akiwasilisha majumuisho hayo ya mwisho wakili wa serikali, Boniface Stanslaus aliiomba mahakama iwaone washtakiwa hao wana kesi ya kujibu. SOURCE: MWANANCHI

Comments

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri